Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba imetangaza majina mawili ya Juma Nkamia na Multaza Mangungu kuwania nafasi ya Mwenyekiti ambayo imeachwa wazi na Swedi Mkwabi aliyejiuzulu mwaka jana.
Mwenyekiti wa Kamati hivyo, Boniface Lyamwike amesema waliochukua fomu wagombea 11 lakini waliorejesha ni saba ambao ni Hassan Dalali, Rashid Shangazi, Nkamia, Mohammed Soloka, Bito Mwakisu, Mangungu na Hamis Tika.
Hata hivyo majina matano yaliingia kwenye kinyang'anyiro hicho lakini watatu walijitoa wenyewe na kubaki Nkamia na Mangungu
Lyamwike amesema kampeni zitaanza kesho na zitadumu kwa siku 21 kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Februari 7.
ADVERTISE HERE