Mchakato wa Mabadiliko Yanga kukamilika May

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2020
Mchakato wa Mabadiliko Yanga kukamilika May

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo utakamilishwa mwezi May

Wapenzi, Wanachama na Mashabiki wa Yanga wamekuwa na shauku kubwa kuona jambo hilo likitokea

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amewataka Wanachama wa klabu hiyo wakae tayari kupokea mabadiliko hayo

"Tumeunda Kamati ambayo inasimamia mchakato huo, tunashukuru kila kitu kinaenda sawa, " amesena

"Tumekuwa tukipokea maoni, ushauri na mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali. Muhimu zaidi tumepata nafasi ya kwenda kujifunza kwa wenzetu waliofanikiwa"

"Lengo letu ni kuwa na mfumo ambayo utaifanya Yanga isimame na kuweka historia ya Mafanikio"

Baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo mwaka uliopita, Dk Mshindo Msolla alitangaza suala la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kuwa kipaumbele chake cha kwanza

Hii si mara ya kwanza kwa Yanga kujaribu kubadili mfumo wake wa uendeshaji kuwa kampuni

Tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000 Yanga imejaribu mara kadhaa bila ya mafanikio, mivutano baina ya wanachama ikikwamisha zoezi hilo

Lakini hitaji la mabadiliko wakati huu limekuwa kubwa miongoni mwa Wanachama wa klabu hiyo

Kama mpango huo utafanikiwa, Dk Msolla ataingia kwenye historia ya klabu hiyo kwa kufanikiwa kumaliza mchakato huo ambao watangulizi wake hawakufanikiwa kuukamilisha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’