Simba imebakiwa na hatua moja tu kutinga fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi usiku wa leo wakitarajiwa kucheza na Namungo Fc
Kocha Selemani Matola amepania kushinda taji la kwanza akiwa kocha wa Simba, huu ni mchezo ambao Simba inahitaji ushindi iweze kutinga fainali
Aidha upo uwezekano wakakutana na watani zao Yanga kwenye mchezo wa fainali kama Yanga watashinda mchezo wao wa nusu fainali ambao utapigwa mapema dhidi ya Azam Fc

Simba ndio timu pekee iliyoshinda mechi zake zote mbili katika hatua ya makundi, wanafukuzia rekodi ya kushinda mechi zote katika michuano hiyo mwaka huu
Mchezo utapigwa kuanzia saa mbili na robo usiku
ADVERTISE HERE