Baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Simba tayari imeinufaisha Tanzania mapema tu baada kupanda nafasi ya 12 katika viwango vya soka vya CAF
Hii ina maana kama msimamo utabaki hivyo, msimu ujao Tanzania itatoa wawakilishi wanne kwenye michuano ya vilabu barani Afrika (Ligi ya mabingwa 2, kombe la Shirikisho 2)
Idadi ya alama za Tanzania zinaweza kuongezeka kulingana na matokeo ambayo Simba itapata katika hatua ya makundi
Na pengine zitaongezeka zaidi kama Namungo Fc nao watafanikiwa kutinga makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho wakiwa hatua moja tu wakisubiri droo ya raundi ya mwisho ya mtoano kuelekea makundi
Wale zomea zomea Fc, wawashukuru mabingwa wa nchi kwani bila ya hivyo pengine mwakani tena wasingepanda ndege....!
