Baada ya mapumziko ya siku mbili, kikosi cha Simba kinarejea mazoezini leo kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Fc Platinum ambao utapigwa Jumatano, Januari 06, uwanja wa Benjamin Mkapa
Mchezo huo uliopewa kauli mbiu ya War In Dar (WIDA) ni lazima Simba ishinde kwa angalau mabao 2-0 ili iweze kutinga moja kwa moja hatua ya makundi
Uongozi wa klabu ya Simba uliwapa wachezaji mapumziko baada ya mchezo dhidi ya Ihefu, mchezo ambao Simba ilifunga mwaka 2020 kibabe kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0
Sasa akili na Mawazo ya Wanamsimbazi zimeelekezwa kwa Wazimbabwe Fc Platinum kuhakikisha hawatoki kwa Mkapa
ADVERTISE HERE