Platinum Fc imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Winga wa Platinum Chikwende ndiye aliyefunga bao pekee la wenyeji akiwazidi ujanja walinzi wa Simba
Simba waliuanza mchezo huo taratibu wakicheza kwa tahadhari
Kipindi cha pili Simba ilikuwa bora zaidi lakini safu ya ulinzi ya Platinum ilikuwa kikwazo kwa Simba kupata bao la kusawazisha
Ni matokeo ambayo sasa yanailazimu Simba kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa marudiano ambao utapigwa jijini Dar es salaam wiki mbili zijazo
Ushindi wa kunzia mabao mawili utaihakikishia Simba kutinga hatua ya makundi
ADVERTISE HERE