Uongozi wa klabu ya Yanga umevunja kambi na kuwaruhusu wachezaji kurudi makwao baada ya Serikali kusitisha shughuli zote za michezo kwa muda wa siku 30 kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema pamoja na kuwa klabu ilikuwa imeanza kuchukua hatua mapema lakini kufuatia tamko hilo la Serikali, wamewaruhu wachezaji kurudi makwao
Aidha Bumbuli amesema Kocha Mkuu Luc Eymael ametoa program maalum za mazoezi kwa mchezaji mmoja mmoja
Kila mchezaji anapaswa kufanya program hiyo kwa muda wote wa siku 30
ADVERTISE HERE