Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez amewahamasisha wachezaji kuhakikisha leo wanawapa furaha Wanamsimbazi kwa kuibuka na ushindi huko nchini Zimbabwe
Saa kumi jioni ya leo, Simba itashuka katika uwanja wa Taifa wa Harare kuikabili Platinum Fc katika mchezo wa ligi ya mabingwa
Barbara amesema ana imani kubwa na wachezaji wa Simba, siku hii ni muhimu kwao kuipa sifa klabu yao pamoja na Taifa lao la Tanzania
"Mashujaa wetu, Simba Sc, tunaamini mtafanya vizuri sababu nia tunayo na uwezo tunao.Nyie ni timu imara, Mwenyezi Mungu atusimamie ile turudi na ushindi nyumbani, InshaβAllah," aliandika Barbara kwenye ukurasa wa mtandao wake wa kijamii
Mashabiki wa Simba kote nchini wanasubiri kwa hamu mtanange huo ambao utapigwa saa tisa kwa saa za Zimbabwe ambako huku Tanzania ni saa kumi jioni
Mchezo utarushwa mbashara na Azam Sport