Nyota kadhaa wa Yanga watakuwa hawana mikataba mwishoni mwa msimu huu hatama yao ikibaki mikononi mwa kocha Luc Eymael
Mkongwe Kelvin Yondani ambaye hivi karibuni aliingia kwenye mgogoro na kocha Luc Eymael anaongoza orodha ya wachezaji hao ambao mikataba yao inamalizika
Lakini pia yumo Andrew Vicent Chikupe ambaye amekosa karibu nusu nzima ya msimu huu baada ya kufanya mgomo akishinikiza alipwe madeni yake ya miaka ya nyuma
Pia wamo mlinda lango Ramadhani Kabwili, Mohammed Issa 'Banka', Said Juma Makapu, Feisal Salum, Jaffar Mohammed, Ally Ally, Mrisho Ngasa na Raphael Daudi
Kwa upande wa wachezaji wa kigeni orodha inaongozwa na David Molinga ambaye upo uwezekano akaondoka mapema zaidi Yanga kutokana na matukio ya utovu wa nidhamu
Wengine ni Erick Kabamba na Yikpe Gnamien ambao inaelezwa pamoja na kupewa mikataba ya muda mrefu, waliwekewa vipengele vya kutathmini viwango vyao ndani ya miezi sita na kama hawatafikia malengo mikataba yao inaweza kuvunjwa
Ni kipengele cha aina hiyo ambacho kiliwafanya Sadney Urikhob na Juma Balinya waondoke