Mabingwa wa Taifa hili Simba Sc jioni ya leo watakuwa na majukumu ya Kitaifa kule nchini Zimbabwe watakaposhuka dimbani kuikabili Platinum Fc katika mchezo wa ligi ya mabingwa
Mchezo huo ni wa raundi ya kwanza, hatua moja kuelekea makundi, utapigwa kuanzia saa kumi jioni
Simba iko Zimbabwe tangu Ijumaa iliyopita, wakifanya maandalizi kabambe kuelekea mchezo huo
Jana vijana wa Sven Vandenbroeck walikamilisha maandalizi ya mwisho katika uwanja wa Taifa wa Harare
Kikosi cha Simba leo kinahitaji ushindi au hata matokeo ya sare, muhimu zaidi ni Simba kufunga bao la ugenini ambalo linaweza kuwarahisishia kazi katika mchezo wa marudiano ambao utapigwa jijini Dar es salaam wiki mbili baadae
Akizungumza baada ya mazoezi ya mwisho jana, Sven alisema wachezaji wote wako katika hali nzuri isipokuwa nahodha John Bocco na mlinda lango Aishi Manula ambao ni mjaeruhi
Dua za Wanamsimbazi na Watanzania wazalendo ziko pamoja na Simba, hakuna shaka Mnyama ataunguruma huko Zimbabwe
Kila la kheri Simbam kila la kheri mabingwa nchi..