Sven awapongeza wachezaji ushindi dhidi ya KMC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Dec 2020
Sven awapongeza wachezaji ushindi dhidi ya KMC

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema vijana wake walipambana katika mchezo dhidi ya KMC jana, ushindi ni matokeo waliyostahili

Aidha Sven amesema walifahamu mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa kuwa KMC ni moja ya timu bora kwenye ligi msimu huu

"Niliwaambia wachezaji kwamba hautakuwa mchezo rahisi kupata matokeo, walipambana na nimefurahishwa kwa sababu tumepata pointi tatu muhimu, " alisema Sven

"Sijali, tumeshinda. Ikiwa ilikuwa ni kuotea au la, penati au si penati, tumeshinda. Sijali, hayo mengine ni mazungumzo, yanabakia kuwa mazungumzo ya vyombo vya Habari. Nimefurahishwa na matokeo ya 1-0 na juhudi zilizooneshwa na wachezaji wangu," aliongeza Sven

Meedie Kagere ndiye aliyefunga bao la Simba kupitia mkwaju wa penati kwenye dakika ya 77 baada ya mwamuzi Elly Sassie kutoa penati hiyo kutokana na tukio la winga wa KMC Hassan Kabunda kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’