FT : Simba 1-0 KMC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Dec 2020
FT : Simba 1-0 KMC

Bao la dakika ya 77 lililofungwa kwa mkwaju wa penati na Meddie Kagere 'MK14' limetosha kuihakikishia Simba ushindi muhimu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Mwamuzi Elly Sassie alitoa mkwaju wa penati baada ya winga wa KMC Hassan Kabunda kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari

Simba iliingia katika mchezo huu ikihitaji alama tatu. Kipindi cha kwanza Simba ilikuwa bora lakini haikuwa katika kasi ambayo mashabiki wameizoea

Akiwa na hesabu za mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Platinum Fc, kocha Sven Vandenbroeck alifanya mabadiliko wakati wa mapumziko akiwatoa nahodha John Bocco na mlinda lango Aishi Manula na nafasi zao kuchukuliwa na Kagere na Beno Kakolanya

Sven ameendelea kuuamini mfumo wake wa kutumia mshambuliaji mmoja licha ya ukosoaji anaopata kutoka kwa wadau wa Simba

Muhimu zaidi mabingwa wameendelea kusogea juu kileleni sasa wakifikisha alama 32, alama tano nyuma ya Yanga ambayo pia imecheza mchezo mmoja zaidi

Simba haitakuwa na mchezo wa ligi wikiendi hii kwani wanatarajiwa kusafiri nchini Zimbabwe tayari kwa mchezo dhidi ya Platinum Fc ambao utapigwa Disemba 22

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’