Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wataondoka jijini Mbeya mchana wa leo kurejea Dar es salaam tayari kwa mchezo wa ligi kuu unaofuata dhidi ya KMC
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Jana Simba ilipata ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, matokeo ambayo yaliwapandisha mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi
Baada ya mchezo dhidi ya KMC, Simba itasafiri nchini Zimbabwe kuikabili Platinum Fc kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa raundi ya kwanza
ADVERTISE HERE