Mshuti wa Morrison ungenvunja kiuno Manula

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Mar 2020
Mshuti wa Morrison ungenvunja kiuno Manula

Mlinda mlango wa JKT Tanzania, Aboubakar Barwany amesema kipa yeyote duniani asingeweza kuokoa mpira wa ‘frii-kiki’ uliopigwa Bernard Morrison ‘BM33’ katika pambano la Yanga na Simba lililopigwa Jumapili iliyopita.

Morrison alipiga mpira huo uliopita juu ya ukuta wa Simba na kwenda kuingia wavuni kupitia ‘anapotagia ndege’na kuipa Yanga uahindi wa kwanza wa ‘Dabi ya Kariakoo’ tangu 2016.

Alisema hata kama kipa Aishi Manula angeweza kuucheza mpira huo basi sasa hivi angekuwa anauguza majeraha kwani Morrison aliupigwa sehemu mbaya sana.

Barwany alisema kipa yeyote kamwe asingeweza kucheza faulo ile kwani Morrison alitumia akili nyingi kupiga ‘frii-kiki’ ile kwani aliwadanganya mabeki hadi Manula wasijue atapigia upande upi.

"Unawezaje kucheza ule mpira na kama Manula angeufuata na kupangua basi asingeweza kuendelea na mechi kwani angeumia kwa sababu Morrison aliupigia sehemu mbaya sana na angeweza kujigonga kwenye mlingoti na kuumia,” alisema Barwany

Alisema hata hivyo Manula anahitaji pongezi kwani aliweza kuufata mpira huo na kwamba kwa jinsi ulivyopigwa, makipa wengi huishia kuutazama tu na kuganda sakafuni kama vile wamepigiliwa misumari.

“Kwangu nampongeza kipa kwani alijaribu kwa uwezo wake wote kuufuata ule mpira lakini haikuwezekana. Kikubwa mashabiki wa soka wajue lile bao anafungwa kipa yeyote duniani na wasije kumlaumu kabisa Manula,” alisema kipa huyo.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’