Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeiruhusu klabu ya Simba kuongeza wachezaji watano wa kigeni kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Baada ya CAF kuviruhusu vilabu vinavyoshiriki michuano yake msimu huu kusajili mpaka wachezaji 40, Simba iliomba mwongozo wa TFF ikiomba ipewe ruhusa ya kusajili nyota 10 wa kigeni kukiboresha kikosi chake
Hata hivyo TFF imewaruhusu mabingwa hao wa nchi kuongeza wachezaji watano wa kigeni ambao watashiriki michuano ya ligi ya mabingwa huku nafasi nyingine tano wakitakiwa kusajili wachezaji wazawa
Simba itaanzia ugenini kampeni ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu kule nchini Nigeria dhidi ya Plateau United
Mchezo huo utapigwa Novemba 28
ADVERTISE HERE