Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' leo alipata ugeni ofisini kwake alipotembelewa na kiungo mshambuliaji Hassan Dilunga
Dilunga ni mmoja wa wachezaji wa Simba walioramba mikataba minono mwanzoni mwa msimu huu
Wanamsimbazi hawawezi kusahau heshima aliyowapa mwaka 2018 pale assist yake ilipoipeleka Simba hatua ya makundi ligi ya mabingwa, akimsaidia Chama kufunga bao muhimu kwenye dakika za lama salama mchezo dhidi ya Nkana Fc
Msimu huu wana kazi ya kuhakikisha wanarejea kile walichokifanya misimu miwili iliyopita
Shughuli itaanza mwishoni mwa mwezi huu nchini Nigeria katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali dhidi ya Plateau United
ADVERTISE HERE