Tatizo la Singida United sio ukata - Mwigulu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
20 Feb 2020
Tatizo la Singida United sio ukata - Mwigulu

Rais wa klabu ya Singida United Dk Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Mwanachama wa Yanga, amesema usajili wa vijana wengi waliofanya umechangia timu hiyo kukosa makali msimu huu na sio ukata kama inayoripotiwa

Dk Mwigulu ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi amesema timu yake haina tatizo la fedha na wana usafiri mzuri kuliko wa timu ya Simba SC ya Dar es Salaam

Dk Nchemba amesema kama wangekuwa na tatizo la fedha jamii ingeshasikia siku moja wamekwama hotelini na kwamba, wachezaji wa timu hiyo hawajawahi kulala njaa au kula mlo mmoja.

Amesema wachezaji wa Singida United wanapata mishahara kama inavyostahili na kwamba wanafanya vibaya kwa sababu walisajili vijana wasio na uzoefu.

“Na wana usafiri bora kuliko hata wa Simba, usafiri bora kuliko hata ule wa Simba sisi tulichokosea tu ni kwamba tulichukua vijana ndio maana nimeshajua kwa nini Simba wanasajili wazee"

"Ndio maana na mimi nikaona nimlete Haruna Moshi na Chuji…aah nimeshaona bwana kwa nini jamaa wanaleta veterani, Kagere yule tulicheza nae Umisseta (Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania) wakati ule Waziri wao akiwa Saitoti sisi wa kwetu huku akiwa Kapuya”amesema Nchemba alipozungumza wakati wa kipindi cha michezo cha Sports Arena kinachorushwa na redio ya Wasafi FM.

Mwanasiasa huyo amesema anaamini timu ya Singida United itapambana isishuke daraja.

Amesema hashangazwi na matokeo inayopata timu hiyo kwa kuwa yanatokana na ugumu wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara.

Kwa mujibu wa Dk Nchemba tangu ligi ilipoanza amekuwa akipambana kwa ajili mafanikio ya timu hiyo na si kweli kuwa amejiweka kando kwa sababu ya matokeo mabaya inayopata.

Amesema Singida United inapata matokeo mabaya kwa sababu raundi ya kwanza ilisajili wachezaji wasio na uzoefu wakakuta ligi ngumu.

"Raundi ya pili tumebadilisha kikosi sasa hakijaelewana we utaona kwamba mechi hizi zote walizocheza mchezaji wa zamani anakuwa mmoja ama wawili kwa hiyo timu haijaunganika sasa ndio maana timu huwa zinafanya pre season maana huwa ili timu ijuane sasa sisi timu wanajuana ndani ya mechi ndo maana inakuwa shida"amesema.

Singida United iko nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 11 tu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →