Beki kisiki wa Simba Joash Onyango ameondolewa katika kambi ya timu ya Taifa ya Kenya inayojiandaa na mechi za kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2021 dhidi ya Comoro baada ya kuumia goti
Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amethibitisha kuwa Onyango ameondolewa timu ya Taifa huku akikanusha taarifa zilizosambaa kuwa alikutwa na maambukizi ya virusi vya COVID-19
"Nimezungumza na staa wetu Joash Onyango, si kweli kuwa anaumwa Corona ameumia goti na anaendelea vizuri" amesema Barbara
ADVERTISE HERE