Mshambuliaji Ditram Nchimbi ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao keshokutwa Jumanne watakuwa dimbani kuikabili Polisi Tanzania kwenye mchezo wa ligi kuu
Yanga tayari imewasili mkoani Kilimanjaro kuelekea mchezo huo ambao utapigwa uwanja wa Chuo cha Ushirika
Nchimbi alijiunga na Yanga akitokea klabu ya Polisi Tanzania ambayo alikuwa akiitumikia kwa mkopo akitoka Azam Fc
Mshambuliaji huyo maarufu 'Duma', alikuwa tegemeo kikosi cha Polisi Tanzania akifunga mabao yote matatu kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga
Lakini keshokutwa atarejea hapo Ushirika lakini akiwa ndani ya uzi wa Yanga kuwakabili waajiri wake hao wa zamani

ADVERTISE HERE