Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amewataka wachezaji kuhakikisha wanaipa Simba heshima inayostahili kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Ruvu Shooting leo
Manara amesema leo Simba haitakuwa na sababu ya kutopata ushindi kutokana na ubora wa kikosi chake
Amesema pamoja na kuwa mpira una matokeo matatu, lakini leo ni lazima lipatikane tokeo moja tu la ushindi upande wao
"Hakuna utetezi leo, hakuna mpira una matokeo matatu, kwetu leo mpira una tokeo moja tu, ushindi"
"Ndio, sisi ni mabingwa, Simba ndio timu bora nchi hii, lazima tuhakikishe tunarejea kibingwa, nawaaminia Wanaume na nnajua nini mtafanya leo, tunachofanya ni kuendelea kuwaombea kwa Mungu," Manara ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
ADVERTISE HERE