Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Tanzania Prisons kwa kufungwa bao 1-0, mabingwa wa nchi Simba sasa wameelekeza nguvu zao kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting
Mchezo huo utapigwa Jumatatu, Oktoba 26 kwenye uwanja wa Uhuru
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema wamesahau matokeo ya mchezo dhidi ya Prisons, akili wameihamishia mchezo dhidi ya Ruvu Shooting
"Mpira una matokeo matatu, lazima moja kati ya matokeo hayo litokee, hii ni ligi baada ya mchezo mmoja kwisha mchezo mwingine unafuata. Tunajiandaa kufanya vizuri mchezo unaofuata," amesema
ADVERTISE HERE