Mabingwa wako tayari kuikabili Prisons

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Oct 2020
Mabingwa wako tayari kuikabili Prisons

Mabingwa wa nchi Simba tayari wako ndani ya Mji wa Sumbawanga wakihesabu masaa kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa kesho Alhamisi kwenye uwanja wa Nelson Mandela

Simba itaingia katika mchezo huu ikiwa na hesabu ya kuondoka na alama zote tatu ili kuhakikisha wanasogea karibu ya vinara Azam Fc ambao wanaonekana kuwa 'wamoto' msimu huu

Azam Fc inaongoza ligi ikiwa na alama 21 baada ya kushinda michezo yake yote saba

Ni alama nane juu ya Mabingwa watetezi Simba wenye alama 13 lakini pia wakiwa na mechi mbili mkononi

Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema wanafahamu mchezo dhidi ya Prisons hautakuwa mwepesi lakini kama mabingwa, wana kila sababu ya kushinda mchezo huo

"Mchezo wetu wa Oktoba 22 dhidi ya Tanzania Prisons sio mwepesi kwani tunakutana na timu ngumu na yenye wachezaji wapambanaji muda wote.

"Unajua timu za majeshi zenyewe muda wote zipo fiti hapo unaweza kujua Simba tunakwenda kukutana na timu ya aina gani.

"Kwa kuwa sisi ni mabingwa watetezi basi lazima tuingie kibingwa na tucheze tukiwa ni mabingwa watetezi, mashabiki wetu watupe sapoti ili timu ipate matokeo kwani tunahitai ushindi," alisema Manara

Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck ataingia katika mchezo huo huku akiwakosa baadhi ya nyota wake muhimu kutokana na sababu mbalimbali

Washambuliaji Meddie Kagere na John Bocco ni majeruhi wakati kiungo Clatous Chama na beki Paschal Wawa walipewa ruhusa kurejea katika nchi zao kuhuisha paspoti zao

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’