Yanga uso kwa uso dhidi ya Mtibwa Sugar uwanja wa Taifa leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Feb 2020
Yanga uso kwa uso dhidi ya Mtibwa Sugar uwanja wa Taifa leo

Baada ya mapumziko ya wiki nzima, kikosi cha Yanga leo kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikaribisha Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Baada ya kushinda michezo miwili iliyopita, kikosi cha Luc Eymael kitahitaji kuendeleza wimbi hilo la ushindi ili kuhakikisha wanaendelea kubaki kwenye mbio za kuwania ubingwa

Yanga imeshuka dimbani mara 15 na kujikusanyia alama 28 ambazo ni alama 19 pungufu ya vinara wa ligi hiyo Simba wenye alama 47

Hata hivyo Simba imecheza mechi tatu zaidi ya Yanga

Mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar hautakuwa mwepesi kutokana na kuimarika kwa mabingwa hao wa kombe la Mapinduzi

Kwenye mchezo wao uliopita, Mtibwa Sugar walipata matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam Fc katika mchezo ambao ulipigwa uwanja wa Taifa

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa VIP A ni Tsh 15,000/- VIP B na C ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’