Mugalu aahidi alama tatu Rukwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Oct 2020
Mugalu aahidi alama tatu Rukwa

Mshambuliaji wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Prisons utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Mandela, mjini Sumbawanga.

Mcongomani huyo aliyetua Simba akitokea klabu ya Lusaka Dynamos ya Zambia, amesema anatambua mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao hao, japo hilo haliwezi kuwazuia kupata ushindi.

"Tunajua mchezo utakuwa mgumu, wenyeji wetu watapambana, nasi tunakwenda kupambana tupate ushindi ambao utatuweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kupigania ubingwa wetu wa ligi," alisema Mugalu.

Aidha, Mugalu alisema kuwa anafurahi kucheza katika Ligi ya Tanzania ambao ni miongoni mwa ligi zenye ushindani mkali unaosaidia kuwa na wachezaji wengi wazuri.

"Nimefurahia kuona ligi ina ushindani mkali, kila timu inapambana ipate matokeo, nami na wachezaji wenzangu tunaipambania timu yetu ya Simba iweze kufanya vizuri na hatimaye kutwaa ubingwa"

Mugalu anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Simba kwenye mchezo huo Meddie Kagere na John Bocco ikielezwa watakosekana kutokana na kuwa majeruhi

Nyota wengine wanaoweza kukosa mchezo huo ni pamoja na Mzambia Clatous Chama na Paschal Wawa ambao walipewa ruhusa kurejea katika nchi zao kuhuisha vibali vyao

Aidha beki Ibrahim Ame naye anatajwa kukabiliwa na matatizo ya kifamilia

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’