Tarimba 'awachana' TFF, Bodi ya Ligi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Feb 2020
Tarimba 'awachana' TFF, Bodi ya Ligi

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kampuni ya Sportpesa Abbas Tarimba ameeleza kushangwaza na TFF kutomchukulia hatua Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mguto ambaye juzi alikiri bodi yake kusahau kuipangia Yanga ratiba

Tarimba ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga ameeleza kushangazwa hatua zozote kutochukuliwa kwa kiongozi huyo ikiwemo yeye mwenyewe kujiuzulu

"Inakuwaje kiongozi unatoka hadharani unasema umesahau kuipangia timu mechi na bado ukaendelea kuwa ofisini?," alihoji Tarimba

"Nakumbuka TFF waliwahi kumchukulia hatua Afisa wao mmoja ambaye alifanya kosa la kubadili muda wa mchezo wa ligi kutoka saa moja jioni kwenda saa kumi, lakini huyu aliyekiri kufanya kosa kubwa zaidi yupo tu"

Aidha Tarimba pia amezungumzia suala la waamuzi ambao wameendelea kufanya makosa yaleyale kila siku kuwa wanaharibu taswira ya soka la Tanzania

"Itafika wakati mashabiki wataacha kwenda viwanjani kama mambo haya yataendelea kufumbiwa macho. Unakwenda kufanya nini uwanjani wakati unafahamu hakuna uhakika wa utolewaji wa haki miongoni mwa timu zinazoshindana"

"Hili pia linatoa taswira mbaya kwa watu wanaofuatilia soka la Tanzania huko nje kwani lazima ifahamike haya yanayofanyika yanaonekana kote duniani. Mfano ukiingia Youtube leo popote ulipo duniani utaona goli la Simba walilofunga dhidi ya Namungo ambalo linalalamikiwa"

Katika hatua nyingine, Tarimba amewashauri viongozi wa soka nchini kuweka msimamo kwa ukiukaji wote wa kanuni ambao unafanyika kwenye ligi

"Viongozi wanaweka msimamo kwenye baadhi ya masuala lakini mengine hawana habari nayo. Nakumbuka kijana wetu wa timu ya Taifa Ditram Nchimbi alikanyagwa kwa makusudi kabisa na mlinzi wa Simba Paschal Wawa. Tukio lile kila mmoja ameliona lakini hakuna kiongozi yeyote aliyekemea wala hatua yoyote kuchukuliwa"

Tarimba ametahadharisha kuwa kuendelea kwa matukio hayo kunaweza kuwa athari kubwa zaidi ikiwa ni pamoja na mashabiki kuacha kwenda viwanjani na pia wawekezaji kuamua kuondoka kwa kuwa wanaona mchezo wa mpira wa miguu haupewi heshima yake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’