Kesho Jumamosi, Oktoba 17 2020 mabingwa wa nchi Simba watakuwa uwanja wa Azam Complex Chamazi kupepetana na Mlandege kwenye mchezo wa kirafiki
Viingilio vya mchezo huo ambao utapigwa kuanzia saa 11 jioni, VIP ni Tsh 7,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Simba itatumia mchezo huu kuwanoa vijana wake kuelekea mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Oktoba 22 mkoani Rukwa
Wababe hao wa soka nchini hawana ratiba ya mechi za ligi mwishoni mwa wiki baada ya mchezo wao dhidi ya Yanga uliokuwa upigwe Jumapil, Oktoba 18 kupigwa kalenda
ADVERTISE HERE