Kikosi cha Yanga leo kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa siku ya Jumapili, Februari 02 2020
Baada ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons Jumapili iliyopita, wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko ya siku mbili ambapo walirejea mazoezini jana
Wapinzani wao Mtibwa Sugar tayari wako jijini Dar es salaam ambapo leo watacheza na Azam Fc ukiwa ni mchezo wa ligi
Kikosi cha Yanga kimepata mapumziko ya wiki nzima tangu walipocheza Jumapili iliyopita, watashuka tena dimbani Jumapili ijayo
ADVERTISE HERE