Baada ya kumaliza kazi iliyowapeleka mkoani Dodoma jana kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania, kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba kiliondoka jana mkoani Dodoma ambapo msafara umelala mkoani Morogoro
Mapema leo Machampioni hao wa Taifa hili wanatarajiwa kuianza safari ya kurejea jijini Dar es salaam kuanza maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 18
Hata hivyo Simba itaanza maandalizi hayo pasipo kuwa na wachezaji wake 12 ambao wanatarajiwa kuondoka kujiunga na timu za Taifa kwa ajili ya michezo ya Kimataifa ya kirafiki ambayo itapigwa wiki ijayo
Nyota wa Simba walioitwa timu za Taifa ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Jonas Mkude, Hamis Ndemla, John Bocco na Mzamiru Yassin
Wengine ni Luis Miquissone, Clatous Chama, Larry Bwalya, Joash Onyango na Francis Kahata