Faini kama zote Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jan 2020
Faini kama zote Yanga

Kamati ya Uendeshaji na usimamizi wa ligi 'Kamati ya Saa 72' imekutana juzi Januari 20 na kutoa adhabu mbali mbali huku klabu ya Yanga wakiwa wahanga wakubwa.

Katika mchezo namba 22 kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Samora mkoani Iringa timu zote zimepigwa faini ya shilingi laki tano kila moja kutowasilisha vikosi vyao ambavyo vilotakiwa kucheza kwa mujibu wa kanuni.

Mchezo namba 17 kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga wachezaji Kelvin John na Majaliwa Shaban wa City na Mrisho Ngasa, Ramadhan Kabwili pamoja na Cleofas Sospeter wamefungiwa mechi tatu na faini ya shilingi laki tano kila mmoja baada ya kugoma kutoka uwanjani wakati wa mapumziko.

Mchezo namba 89 kati ya Azam FC dhidi ya Yanga, kocha mkuu wa Yanga, Luc Eymael amepewa onyo kali baada ya kutoa maneno yenye viashiria vya ubaguzi wa rangi baada ya mwamuzi Hans Mabena kugoma kumpa mkono baada ya mchezo kati ya Azam Fc dhidi ya Yanga

Mchezo namba 130 kati ya Simba dhidi ya Yanga, klabu ya Yanga imetozwa faini ya shilingi laki tano baada ya mashabiki wake kurusha chupa za maji na kuwatolewa lugha chafu waamuzi wa mchezo.

Pia katika mchezo huo Yanga imepigwa faini ya shilingi laki mbili baada ya kutotumia chumba maalum cha kubadilishia nguo kinyume na kanuni.

Wachezaji wa Yanga, Ngasa, Kabwili na Sospeter wanaweza kucheza mechi ya leo dhidi ya Singida United kwakua barua ya kufungiwa kwao itatumwa baada ya mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika leo mchana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’