Ligi Kuu ya Vodacom leo imeingia mzunguuko wa nne kwa mechi mbili kupigwa kule mkoani Kagera na Mbeya
Kagera Sugar imezinduka kutoka usingizini baada ya kufanikiwa kuwalaza vinara wa ligi hiyo KMC kwa bao 1-0
Matokeo hayo yanazipa nafasi Azam Fc na Simba kuongoza ligi kama zitashinda mechi zao hapo kesho
Nayo Mbeya City imeendelea na mwenendo wa kugawa pointi baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Namungo Fc
Mbeya City sasa imekamilisha michezo minne bila ya kuambulia pointi wala kufunga bao
Ligi hiyo itaendelea kesho Jumamosi kwa mechi nyingine tatu kupigwa
Polisi Tanzania inatarajiwa kucheza na Dodoma jiji katika mchezo utakaopigwa mapema kisha kufuatiwa na mchezo kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Azam Fc
Mabingwa watetezi Simba wao watashuka dimbani saa moja usiku kuikabili Gwambina Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Kama Azam Fc itakosa ushindi dhidi ya Prisons na Simba ikashinda, basi mabingwa hao wa nchi watarejea rasmi kileleni mwa msimamo wa ligi