Niyonzima aomba radhi, mashabiki wawapa moyo wachezaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jan 2020
Niyonzima aomba radhi, mashabiki wawapa moyo wachezaji

Kiungo Haruna Niyonzima aliwaomba radhi wachezaji wenzake jana baada ya makosa yake kupelekea kufungwa bao la pili katika mchezo ambao Yanga ilifungwa mabao 3-0 na Kagera Sugar

Niyonzima aliyekuwa nahodha wa Yanga kwenye mchezo huo, alipokonywa mpira eneo la hatari wakati alipojaribu kumpiga chenga ya kisigino mchezaji wa Kagera Sugar

Ukiachana na tukio hilo, Niyonzima alikuwa na mchezo mzuri, alionekana kuwahamasisha wenzake wakati timu hiyo ilipokuwa nyuma

Lakini pia mashabiki wa Yanga walionyesha uungwana mkubwa kwa wachezaji baada ya mchezo huo kumalizika

Mashabiki waliojitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru walifanya tukio la aina yake kwa kuweka mstari na wachezaji kupita kati yao huku wakiwapigia makofi

Mashabiki hao ni kama walitoa elimu kwa watani zao Simba ambao juzi waliwazomea wachezaji wao baada ya kupoteza fainali ya kombe la Mapinduzi kwa kufungwa na Mtibwa Sugar bao 1-0

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’