Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema ni klabu ya Azam Fc pekee ambayo inaweza kujaribu kushindana nao katika kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu
Hata hivyo Manara amesema bado wana zaidi ya asilimia 75, kuhifadhi taji lao kwa msimu wa nne mfululizo
Manara ameipa Azam Fc asilimia 24 za kushinda ubingwa wakati watani zake Yanga amewapa asilimia moja tu
Bosi huyo wa kitengo cha habari na Mawasiliano klabu ya Simba yuko katika ziara ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari aliyoianza jana pale Azam Media
ADVERTISE HERE