Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba usiku huu wametakata pale uwanja wa Benjamin Mkapa wakiwafumua Biashara United mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Simba kucheza katika uwanja wake wa nyumbani, hakika wababe hao wa soka nchini, bado hawana mpinzani katika kutandaza soka la kitabuni
Mabao mawili ya Clatous Chama, Meddie Kagere na Chris Mugalu yalitosha kuihakikishia Simba ushindi muhimu katika mchezo ambao walikuwa katika kiwango bora sana


Aidha Sven leo ameona umuhimu wa kumuanzisha Kagere ambaye sasa amefungua akaunti yake ya mabao msimu huu
Ushindi mnono leo umerejesha furaha ya mashabiki ambao hawakufurahishwa na matokeo ya mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar
Burudani bado itaendelea hapo uwanja wa Mkapa wiki ijayo pale Simba itakapoikaribisha Gwambina Fc
Kwa hakika wenye mji wao wamerudi, wengine watafute pa kujificha...!