Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi, Salim Abdallah 'Try Again' amesema kwa usajili walioufanya safari hii wanaamini wanaenda kupeperusha bendera ya nchi vyema kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Try Againi amesema kwa sasa uongozi wa Simba unasimamia kuhakikisha wachezaji wanaandaliwa kwa uaminifu na kwa weledi wa kutoa ushindani kwa timu zingine.
Tray Again amesema malengo yao ni kutinga kwenye hatua ya makundi kwenye michuano hiyo na baada ya hapo wataangalia.
"Dalili ya mvua ni mawingu tumeanza vyema kwa kuchukua Ngao ya Jamii na kwa usajili tuliofanya tunaamini tutapeperusha bendera ya nchi vyema, kwenye ligi ya mabingwa Afrika, kikubwa tunawaanda wachezaji ili tufikie hatua ya makundi ndiyo malengo yetu," alisema Try Again.
Pamoja na kudhamiria kufanya makubwa kimataifa, Try Againi amesema bado wanatamani kufanya makubwa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ili kutetea ubingwa kwa mara ya nne mfululizo
Amewaomba mashabiki wa mabingwa hao wa nchi kuwa watulivu kwenye kipindi ambacho benchi la ufundi linafanya kazi yake ya maandalizi kwa wachezaji wapya na wazamani
Simba imepata tiketi ya kuiwakilisha nchi baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita. Watawakilisha Tanzania kwenye michauno ya CAF msimu ujao pamoja na Namungo FC
Michuano hiyo kwa mwaka huu itaanza mwezi Novemba