Jana baada ya Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla kudai kuwa kesho Jumatatu wanapeleka malalamiko yao rasmi FIFA wakidai kuwa na mkataba halali na winga Bernard Morrison, mwamba huyo kutoka nchini Ghana, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ni kama amewapiga dongo Yanga kuwa huko nako hawataambulia kitu
Morrison jana alionyesha thamani yake kwa kufunga bao pamoja na kutoa asisti kwenye ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Vital'o ukiwa ni mchezo wa Simba Day
Inaelezwa klabu ya Yanga imemjumuisha Morrison kwenye usajili wao, jina lake wakiwa wamelisajili kwenye mfumo wa FIFA (TMS)
Sakata hili linaweza kuwaingiza Yanga wenyewe matatani huko FIFA kama itabainika ni kweli walifoji mkataba huo
ADVERTISE HERE