Kikosi cha Yanga kiko mkoani Mbeya tayari kwa michezo miwili ya ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons
Jioni ya leo mabingwa hao wa kihistoria wamefanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Sokoine ambao utatumika kwenye michezo hiyo
Mchezo wa kwanza utapigwa kesho Jumanne dhidi ya Mbeya City na kisha siku tatu baadae yaani siku ya Ijumaa Yanga itarejea Sokoine kuikabili Tanzania Prisons
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema pamoja na kufahamu kuwa michezo hiyo haitakuwa rahisi, lakini wamejiandaa kuondoka na alama zote sita
ADVERTISE HERE