FT Simba 6-0 Vital'o, Kikosi la kibabe, ushindi wa kibabe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Aug 2020
FT Simba 6-0 Vital'o, Kikosi la kibabe, ushindi wa kibabe

Ni raha tupu kuwa shabiki wa mabingwa wa nchi Simba, hakika ubingwa wa msimu wa nne mfululizo dalili zimeonekana mapemaaa

Ni kutokana na kiwango cha kutisha kilichoonyeshwa na Simba kwenye mchezo Simba Day wakiwafumua Vital'o kutoka Burundi mabao 6-0

Huu ulikuwa ni mchezo maalum kutambulisha kikosi cha mabingwa hao wa nchi kuelekea msimu mpya

Kabla ya mchezo huo kulikuwa na utambulisho wa wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao

Simba imeleta mafundi! Huyu Larry Bwalya, sio mtu mzuri, kiungo fundi anayelifanya soka lionekane kama kitu rahisi sana

Mabosi wa Kamati ya usajili Simba wanastahili pongezi kwa usajili wa fundi huyu kutoka nchini Zambia

Lakini mtukutu Bernard Morrison akiwa amefunga moja ya mabao ya Simba, amedhihirisha kwa nini Yanga bado wanaumia baada ya kuwatosa

Ni mchezaji haswa aliyestahili kuwa ndani ya kikosi cha Simba. Mwenyewe ameonyesha kufurahia zaidi maisha yake ndani ya Simba. Akiweka wazi kuwa Simba ni Chuo Kikuu cha mafunzo ya soka Tanzania pale alipokuwa akitambulishwa

Nyota wengine wapya Chris Mugalu na Charles Ilanfya nao wameanza maisha yao vyema wakipachika mabao katika mchezo huo

Lakini pia ilikuwa siku nzuri kwa nahodha John Bocco ambaye ameendeleza rekodi yake nzuri ya mabao akifunga bao safi kwenye mchezo huo

Mabao mengine yaliwekwa kambani na mwamba wa Lusaka Clatous Chama na Ibra Cadarba, Ajib Migomba

Huu ulikuwa mchezo wa kutambulisha timu ya msimu mpya, ni kama kutest mitambo tu! Mziki kamili haukuachiwa...!

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’