Klabu ya Yanga huenda ikamuweka hadharani kocha wake mpya baada ya mchakato wa kumpata kocha huyo kukamilika
Afisa Mhamasishaji wa timu hiyo Antonio Nugaz amesema mchakato wa kumpata kocha mpya umefikia hatua za mwisho
"Mwenyekiti (Dk Msolla) amenijuza kuwa mchujo wa makocha umefanyika na sasa wamebaki na majina matatu," amesema
"Pengine baada ya dirisha dogo la usajili kufungwa kocha huyo atawekwa hadharani"
Amesema kwa sasa kocha Mkwasa ataendelea na majukumu ya benchi la ufundi ikiwemo maboresho ya kikosi ili kocha mpya atakapokuja akute timu iko imara
ADVERTISE HERE