Wiki ya Mabingwa kuanza kesho Ijumaa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Aug 2020
Wiki ya Mabingwa kuanza kesho Ijumaa

Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kufunguliwa kwa msimu mpya wa Simba Day kuanzia siku ya kesho Ijumaa August 14 2020 mpaka August 22 2020

Akizungumza na Wanahabari katika Mkutano uliofanyika Serena Hotel, Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema tukio la mwaka huu litabeba jina Wiki ya Mabingwa (Champions Week Day)

Manara ametaja Matukio ambayo yatafanyika katika kipindi chote ya shamrashamra hizo;

"Kesho Ijumaa tutazindua nembo mpya ya klabu. Tumeiboresha ili iendane na soko la sasa. Baada ya uzinduzi wa logo mpya tutazindua jezi mpya ya Simba ya msimu. Hii ndio baada ya hapo tunaanza kutanganza wachezaji wapya"

"Jumamosi kuanzia saa 2 asubuhi tutakuwa kwenye fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Salenda. Kama upo mkoani fanya kwenye eneo lako. Jumapili kuanzia saa 6 mchana tutakuwa makao makuu ya klabu kufanya dua"

"Katika kuunga mkono serikali, jumatatu na jumanne kupitia matawi yote nchi nzima. Wanasimba wote tutembelee vivutio vya utalii. Ni siku maalumu Wanasimba kuunga mkono utalii wa ndani."

"Pia jumanne kwa kushirikiana na mdhamini mkuu Sportpesa tutatoa msaada kwa watoto ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na kuwapa jezi. Jumatano, alhamisi na ijumaa ni siku za kuchangia damu."

"Alhamisi tutakwenda Shule ya Uhuru, tutakwenda na wachezaji. Pale kuna watoto wenye mahitaji mbalimbali na klabu itakwenda kuchangia."

"Jumatatu tutatangaza timu ambayo itakuja na viingilio vya mchezo husika. Kwa mara ya kwanza Simba tutatumia viwanja viwili kwenye tukio moja. Tutatumia uwanja wa Mkapa na uwanja wa Uhuru kwa kuweka screen kubwa. Uwanja wa Mkapa peke yake hautoshi."

"Tukio la michezo ambalo linaloongoza nchini ni Simba Day. Mwaka jana tulijaza sana ndio maana mwaka huu tunaomba viwanja viwili. Kilele cha Wiki ya Mabingwa itakuwa jumapili Agosti 23 hapa Serena kufanya sherehe na wageni wetu"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
5h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
11h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
14h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’