Ile hukumu kuhusu mkataba wa winga Bernard Morrison na timu ya Yanga itatolewa leo na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzaia (TFF)
Simba tayari imetangaza kumsajili Morrison baada ya kubaini mchezaji huyo hakuwa na mkataba halali na Yanga
Zacharia Hans Poppe, miongoni mwa wanaotajwa kukamilisha mchakato wa usajili wa Morrison atakuwa pale TFF kushuhudia maamuzi yatakayotangazwa
Poppe ni Mjumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, inaelezwa viongozi wa Yanga walipinga uwepo wake wakidai ana maslahi na Simba

Baada ya hukumu hiyo itafahamika kama mchezaji huyo ataruhusiwa kucheza Simba au la ingawa tayari mabosi wamechungulia mkataba wake na kubaini mapungufu na ndio maana wakamtangaza mapema
ADVERTISE HERE