Dk Ruhago ampa kazi maalum Tariq

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Dec 2019
Dk Ruhago ampa kazi maalum Tariq

Jana Katibu Mkuu wa Yanga Dk David Ruhago ndiye aliyepewa jukumu la kwenda kumpokea mshambuliaji mpya wa timu hiyo Tariq Seif Kiakala aliyetokea nchini Misri

Dk Ruhago alimtaka mshambuliaji huyo kuhakikisha anatimiza malengo ya usajili wake ambayo ni kuifungia timu mabao

"Karibu sana Tariq, umekuja hapa kwa kazi moja tu, kufunga mabao, tunaamini utaifanya kazi hiyo bila wasiwasi," alisema Dk Ruhago

Tariq alikuwa nchini Misri kunako klabu ya Dekernes Fc ambayo hata hivyo hakuweza kuitumikia kwenye ligi baada ya kuchelewa kukamilisha usajili wake

Lakini alifanya vizuri kwenye michezo ya maandalizi ya msimu akiifungia timu hiyo mabao matano na kutoa pasi tatu za mabao

Dekernes Fc ilivutiwa na Tariq baada ya mshambuliaji huyo kufanya vizuri kunako klabu ya Biashara United msimu uliopita

Tariq alihusika kuinusuru Biashara United isiteremke daraja akifunga kwenye mechi tatu kati ya tano za mwisho

Ndiye aliyefunga bao pekee la Biashara United katika ushindi ambao Biashara iliichapa Yanga bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa Musoma

Msimu mmoja nyuma Tariq aliitumikia klabu ya Stand United

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’