Bado siko fiti - Kapombe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Jan 2018
Bado siko fiti - Kapombe
Beki wa Simba, Shomari Kapombe amesema licha ya mashabiki kufurahia ufundi wake uwanjani, lakini anajiona bado hana ufiti wa asilimia mia wa kucheza kiwango anachokihitaji.

Kapombe anasema anajijua jinsi anavyocheza akiwa fiti, jambo linalomfanya aongeze mazoezi ya ziada ili aweze kufanya kitu cha tofauti msimu huu.

"Kiwango ninachokionyesha si cha Kapombe ninayejijua,bado nina safari ya kupambana ili niwe fiti zaidi, kikubwa ni mashabiki kuniombea ili nifikie lengo hilo litakalokuwa faida ya timu," alisema.

"Nashukuru wachezaji wenzangu, walikuwa karibu na mimi , kipindi ambacho nilikuwa nje ya majukumu, ambapo niliweza kupitia mengi kama si kuyapuza nisingekuwa hapa,"anasema.

Anamtaja kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma kwamba alimsaidia kumjenga kisaikolojia na kumwambia atarejea kwa kasi kama ilivyo kwa sasa.

"Djuma ni kocha wa aina yake, hapendi mchezaji ashindwe kufikia ndoto zake, alikuwa ananipa moyo wa kupambana na kuniambia majeraha ni kitu cha kawaida badala yake alinitaka nizingatie mazoezi na kile ninachoambiwa na daktari,"anasema.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’