Obrey Chirwa alipata majeraha madogo katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar na kuibua hofu ya majeruhi zaidi kwenye kikosi cha Yanga.
Wakati Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko wakiwa bado nje, Chirwa jana alifanya mazoezi na kikosi cha Yanga kilichoweka kambi mjini Tabora hivyo kuondoa hofu ya kumkosa mchezo ujao.
Chirwa alicheza vizuri katika mchezo dhidi ya Kagera ambapo alifunga bao moja na kutengeneza moja.
Aidha ushirikiano wake na Ibrahim Ajib uliwavutia wengi akiwemo kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina aliyekusudia kuwatumia tena katika mchezo dhidi ya Stand United Jumapili ijayo.
Leo jioni Yanga itashuka kwenye dimba la Ali Hassani Mwinyi mkoani Tabora kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Rhino Rangers inayoishiriki ligi daraja la kwanza.

ADVERTISE HERE