Mchezo wa ligi kuu kati ya Coastal Union dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Ulikuwa ni mchezo ambao Simba iliutumia kama sehemu ya maandalizi yake kuelekea mchezo wa fainali kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa August 02 huko Sumbawanga
Hata hivyo Simba ilipata pigo kwenye mchezo huo baada ya beki Paschal Wawa kutolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano
Wawa ataukosa mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa Jumapili
Baada ya mchezo huo, mabingwa wa nchi wanaelekea wilayani Moshi kwa ajili ya mchezo wa kuhitimisha msimu



ADVERTISE HERE