Bocco, Kagere wapewa mchongo wa kuvunja rekodi ya Kibadeni

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Jul 2020
Bocco, Kagere wapewa mchongo wa kuvunja rekodi ya Kibadeni

Washambuliaji wa Simba nahodha John Bocco na Meddie Kagere wanaweza kuanza pamoja kesho kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Yanga ambao utapigwa uwanja wa Taifa

Baada ya kukabidhiwa ubingwa wa ligi kuu, mabingwa hao wa nchi wana kazi moja tu kesho, kuhakikisha wanawafunga watani zao ili kunogesha shamrashamra za ubingwa

Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema wamefurahi baada ya kutwaa ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo lakini watafurahi zaidi kama watashinda dhidi ya Yanga

Mwaka 1977 mkongwe Abdallah Kibaden aliweka rekodi ya kufunga mabao matatu 'hat-trik' katika mchezo ambao Simba iliifunga Yanga mabao 6-0

Rekodi hiyo haikuwahi kuvunjwa mpaka wakati huu. Wakati Simba ya sasa inaangaliwa kama moja ya kikosi bora cha muda wote, mashabiki wana shauku ya kuona wanavunja rekodi ya ushindi wa mabao sita iliyowekwa na kina Kibaden

Lakini pia Bocco na Kagere wanaweza kubakia kwenye kumbukumbu vya klabu ya Simba kwa vizazi vijavyo kama wataweza kuifikia rekodi ya Kibaden ambayo inahitaji kuvunjwa baada ya kubakia kwa muda mrefu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’