Kocha Msaidizi wa Simba, Masudi Djuma amesisitiza kuwa mechi yao ya kesho Jumapili, lazima Majimaji ife Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Djuma amempisha Kocha Mkuu mpya, Mfaransa Pierre Lachentre baada ya kutambulishwa rasmi katikati ya wiki hii, lakini alisisitiza kiu yao ni kuona timu yao inapata ushindi wa nne mfululizo mbele ya Majimaji iliyotoka kuzibana Azam na Singida United katika mechi zake za nyumbani kwa kulazimisha sare ya 1-1 kila mchezo.
Djuma alisema Ligi Kuu ndio nafasi pekee kwao ya kubeba ubingwa na hata kukata tiketi ya mechi za kimataifa mwakani, hivyo wapo makini kwa kila mechi.
Γ’β¬ΕNi wakati wa kumwaga jasho na ndio kazi yetu, tunajituma kwa nguvu zetu zote na kumuomba Mungu atujalie afya, hilo ndilo jambo la msingi, tunajipanga vilivyo kuhakikisha tunaendeleza ushindi dhidi ya Majimaji,Γ’β¬Β alisema Kocha Djuma
Simba ipo kileleni mwa msimamo kwa sasa ikiwa na pointi 32 baada ya mechi 14 ikifuatiwa na Azam yenye pointi 30 na Yanga inafuata kwa pointi 25. Leo timu hizo zilizopo nyuma ya Simba zitavaana kwenye Uwanja wa Azam.
Chini ya Djuma, Simba imeshinda mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu ikianza kwa kuipa dozi Ndanda ikiwa kwao kwa mabao 2-0 kabla ya kuinyoa Singida United kwa mabao 4-0 jijini Dar es Salaam na kuizamisha Kagera Sugar kwao kwa mabao 2-0.

ADVERTISE HERE