Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kimewasili salama mkoani Mtwara tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda Fc
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumapili katika uwanja wa Nangwanda Sijaona
Baada ya kutua mkoani humo, mashabiki walijitokeza kwa wingi kuwalaki mabingwa hao mara tatu mfululizo ligi kuu ya Vodacom
Mzambia Clatous Chama alikuwa kivutio zaidi ambapo mashabiki walipagawa kwa shangwe baada ya kumuona
Chama ndio kinara wa pasi za mabao ligi kuu akiwa na asisti tano pia akifunga mabao
Kwa sasa mwamba huyu wa Lusaka ndio kiungo bora wa ushambuliaji
Baada ya mchezo dhidi ya Ndanda, Simba itaelekea mkoani Lindi pale Wilaya ya Ruangwa tayari kwa sherehe za kukabidhiwa ubingwa baada ya mchezo dhidi ya Namungo Fc, Julai 08
ADVERTISE HERE