Gerson Fraga, huyu mkataba mpya ni haki yake

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Jul 2020
Gerson Fraga, huyu mkataba mpya ni haki yake

Kiungo raia wa Brazil Gerson Fraga kwa mara nyingine amedhihirisha kuwa anastahili kuendelea kubaki na mabingwa hao wa nchi baada ya kuonyesha kandanda safi kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Azam Fc

Mchezo huo uliopigwa jana uwanja wa Taifa na kuishuhudia Simba ikicheza kandanda la kitabuni na kuondoka na ushindi wa mabao 2-0, Fraga alicheza kiungo mkabaji 'pacha' na Jonas Mkude

Hata hivyo kocha Sven Vandenbroeck alimpa kazi moja tu, kuvuruga mipango ya Azam Fc pamoja na kukaba na kumpa Mkude uhuru wa kusambaza 'pasi za upendo'

Wengi wanajiuliza ilikuwaje Azam Fc pamoja na ubora wao jana walipoteana mbele ya Simba iliyokuwa imenawili kila mahali? ni kutokana na mbinu hii iliyotumiwa na Sven ambapo Mkude na Chama hawakuwa na majukumu makubwa ya kukaba hivyo kuwafanya wachezeshe timu

Fraga alikuwepo kila mahali, alikaba, alipiga pasi na alifanya kazi zote 'chafu' ambazo kiungo mkabaji anapaswa kuzifanya.  Fraga ni aina ya wachezaji ambao akielekezwa kazi anaifanya kwa ufasaha mkubwa

Itashangaza kama uongozi wa Simba hautamuongeza mkataba mwamba huyu aliyewahi kuwa nahodha wa akina Neymar kwenye timu ya Taifa ya vijana wa Brazil umri chini ya miaka 15

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’