Msolla aipa tano Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Nov 2019
Msolla aipa tano Stars

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema ana matumaini makubwa kuwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itapata ushindi mnono dhidi ya Equatorial Guinea hapo kesho kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya michuano ya Afcon 2021

Akizungumza ofisi kwake alipotembelewa na waandishi wa habari za michezo ikiwa ni moja ya hamasa kuelekea mchezo huo, Dk Msolla amesema Tanzania ina kikosi imara kinachoweza kupata matokeo mazuri

"Tuna timu nzuri, sio jambo rahisi kupata ushindi nchini Sudan na kufanikiwa kutinga fainali za CHAN. Sasa ukiongeza na hawa wachezaji wa nje walioongezeka, tuna nafasi nzuri ya kufanya vizuri"

"Hivyo Kwa niaba ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa klabu ya Yanga, tunaitakia kila la kheri timu yetu ya Taifa, Taifa Stars, katika mchezo wake dhidi ya Guinea ya Ikweta hapo kesho"

Stars itashuka uwanja wa Taifa kesho Ijumaa saa moja jioni kuikabili Guinea ya Ikweta ukiwa ni mchezo wa kwanza kundi J

Stars iko kundi moja pamoja na Guinea ya Ikweta, Libya na Tunisia

Mchezo wa pili utapigwa Novemba 19 nchini Libya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’