Uongozi wa klabu ya Simba umewataka mashabiki kuwa na subira kuelekea shamrashamra za ubingwa kwani wana mchezo muhimu dhidi ya Azam Fc
Simba itacheza na Azam Fc keshokutwa Jumatano katika mchezo wa robo fainali kombe la FA, mabingwa hao wa nchi wakipania kutwaa taji hilo pia
Afisa Habari na Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, amesema kwa sasa wanawekeza nguvu zao kuelekea mchezo huo muhimu
"Mashabiki wetu wawe watulivu, tutakuwa na muda wa kutosha kusherehekea ubingwa wetu. Lakini kwa sasa tuwe pamoja kuhakikisha tunapata ushindi mchezo dhidi ya Azam baadae tutatangaza tarehe rasmi ya kusherehekea ubingwa," amesema Manara
Simba ilitwaa ubingwa jana baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Tanzania Prisons
Matokeo hayo yaliifanya Simba ifikishe alama 79 ambazo haziwezi kufikiwana timu nyingine yoyote